MAJALIWA: MARUFUKU WANAFUNZI KUTOZWA MICHANGO KIHOLELA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Ofisi ya Rais-TAMISEMI ishirikiane na Sekretarieti  za  Mikoa na  Halmashauri zote kufuatilia matumizi na upatikanaji wa taarifa za fedha za Elimumsingi bila ada na zihakikishe wanafunzi hawatozwi  michango kiholela. Vilevile, Mheshimiwa Majaliwa amezitaka taasisi hizo zihakikishe kuanzia sasa maelezo ya kujiunga na shule za umma (Joining Instructions) yanahakikiwa na kupewa idhini